Wabaptist na Umisheni

“Basi enendeni, mkawafundishe mataifa yote, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu: kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru.”
Mathayo 28:19-20

Wabaptist walioko ulimwenguni kote wamejitoa kwa ajili ya umisheni na uinjilisti. Hizi huduma ziko sawa lakini kuna utofauti. Uinjilisti ni pamoja na kueneza injili ya Yesu Kristo kwa watu kwa maneno na kwa matendo. Wakati huo huo ni kweli kwamba kila Mkristo anafanya “umisheni” umisheni ni pamoja na kuwatuma watu kwenda kueneza injili na watu ambao kwa kawaida hawana mawasiliano nao hata kidogo. Kwa kutumwa na Yesu kwa ajili ya umisheni ndio maana halisi ya kumfuata yeye (Yohana 20:21).

Histori ya Umisheni kwa Baptist

Leo hii, Wabaptist ni watu wa umishonari. Hili halikuwa hivyo tangia huko nyuma, haswa kwa kuwafikia watu wa mbali na utofauti wa utamaduni. Wakati fulani, Wabaptist walilenga kuwafikia watu na injili wa jirani,  ambao walikuwa sawa na wao kwa maana ya lugha moja, tamaduni moja na mazingira sawa na yao.

Miaka ya mwishoni mwa 1700, umisheni wa kuifika dunia nzima ulianza kuchukua kasi dani ya Baptist. Kiongozi wa haya mabadiliko alikuwa William Carey, alikuwa Mchungaji kwenye mafunzo huko Uingereza. Carey alikuwa na akili sana kwenye Biblia na lugha zake na kwenye tamaduni mbalimbali za ulimwenguni. Kusoma kwake Biblia kulimfanya kuamini kwamba Mungu alitaka watu kile mahala waliko waisikie injili. Wabaptist wengine waliungana na kuanzisha Baptist Missionary Society (Umoja wa Misheni wa Baptist) mnamo mwaka 1792. Huo umoja ulimhidhinisha Carey kwenda India kama Mmishenari.

Roho ya umisheni alienea Marekani.  Ann Hasseltine Judson na mme wake, Adoniram, pamoja na  Luther Rice ambao hawakuwa Wabaptist awali walichaguliwa kama viongozi wa ushirika wa wamishonari kwenda India mnamo mwaka  1812.  Wakati wako baharini safarini kuelekea India na muda mfupi baadae, walikuwa wanajifunza Biblia kwa kina jambo ambalo likawafanya waamue kuwa Wabaptist.  Rice alirudi marekani ili kuangalia uwezekano wa kutafuta msaada kwa ajili ya kuwasaidia Judson na familia yake ambao waliachwa huko kama Wamisheni. Kwa kiasi kikubwa kutoaka na jitihada zake, Wabaptist walianzia taasis ya kwanza ya kitaifa, ambayo ililenga kwa ajili ya umisheni.

Wabaptist waliendeleza jitihada zao za kuwa wamisheni wa zawa lakini pia walianza kuwa watu wa umisheni ulimwenguni kote. Leo hii, taasis nyingi za Baptist zenye lengo ya kufanya umisheni zipo ulimwenguni kote.

Misingi ya Umisheni

Wabaptist wengi husisitiza kwamba mafundisho ya Biblia hufanya umisheni kuwa jambo la lazima. Sio vinginevyo, na kwamba ushirkiano kwa kujitolea kwa watu na Makianisa kwa ajili ya umisheni huenda sambamba na desturi la Makanisa ya Agano Jipya. Wanaanzisha taasis mbalimbali zenye lengo la kufanya umisheni ulimwenguni kote.

Imani juu ya ukuu wa Kristo ndio msingi kwa Wabaptist. Kristo kama Bwana aliamuru kwamba injili ipelekwe kwa watu wote mahala popote pale (Mathayo 28:18-20; Matendo 1:8). Zaidi ya hapo, Yesu alionyesha mfano wa kazi ya umisheni na alitusihi kumfuata (Mathayo 4:19; 16:24; Luka 9:59; 1 Petro 2:21).

Wabaptist huamini kwamba Biblia ndiyo yenye mamlaka juu ya mafundisho na mwenendo. Biblia ni kitabu cha umisheni, na sio kitabu kwa ajili ya wamishonari. Kwanzia awali kwenye kitabu cha Mwanzo (12:1-3) mpaka kwenye hitimisho kitabu cha Ufunuo (5:9; 7:9) Biblia inaonyesha dhahiri kusudi la Mungu kwamba watu wote duniani wamjue Yeye na kupata wokovu. Ili kueneza habari hizi kuna haja ya Wakristo kutumwa na kueneza neno la wokovu (Warumi 10:8-15). Wanaenenda katika nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 1:8) na ufahamu wa kuwa kila mmoja anaemwamini Yesu ataokolewa (Yohana 3:16; Warumi 10:13).

Biblia pia imeandika wafuasi wa kwanza wa Kristo walidhibitisha umisheni. Walisema injili ni kwa wote, mahala popote. Waliishi kwa maneno yao na matendo. Makanisa ya kwanza yalituma wamisheni ambao walienda mbali sana bila kuangali vizuizi vya mahali, lugha na tamaduni kwa ajili ya kueneza habari njema (Matendo 13). Tunapaswa kufuata mfano wao.

Aina ya kazi za Misheni

Kazi za umisheni ni pamoja na kuwashuhudia watu na kupanda Kanisa pia na pia aina mbalimbali za kutoa huduma kama vile afya, elimu na kilimo. Haya yote lengo lake ni kueneza injili.

Umisheni ulikuwa ukizingatia eneo maalum lenye uhitaji, na Wamishenari walikuwa wakitumwa kufanya kazi kwenye Kanisa la mahali, jimbo, kanda, kitaifa hata ngazi za kimataifa, na hili jambo bado linaendelea hata wakati huu, mazingira sio tena jambo la msingi kwenye umisheni la kuzingatia. Waliko watu ambao bado hawajafikiwa na injili, kuna kazi ya umisheni.

Kwa wakati fulani, Wakristo walitumwa kufanya kazi ya umisheni na ikiwa ndio fani ya maisha yao yote. Fani ya maisha, wamisheni walioajiriwa bado wana umuhimu sana kwenye umisheni. Japo kuwa, watu wengi binafsi wanajihusisha na umisheni, kama vile kwa mkataba wa muda mfupi huenda kutumika na pia kwa kujitolea.

Wakati wa nyuma, ni Makanisa tu ambayo yalikuwa na jukumu la umisheni kwa kutuma msaada wa fedha kwa wamisheni na kulisihii Kanisa kujihusisha na shughuli za umisheni. Mara nyingi hutuma makundi mbalimbali ili kufanya kazi za umisheni. Taasis za dhehebu zipo kwa ajili ya kusaidia hizi jitihada.

Kwa kuongezea kwenye Makanisa, Shule za Biblia, vituo vya kulelea Watoto na vituo vya afya ni sehemu ya kufanya huduma ya umisheni. Taasis za Kibaptist pamoja na wale waliojitolea wanaweza kufanya vizuri zaidi kwenye umisheni.

Wabaptist ulimwenguni kote wanaojishughulisha na umisheni wanazidi kuongezeka. Huko nyuma maeneo mengi yalikuwa yakipokea tu wamisheni, lakini leo hii hayo maeneo pia yanatuma wamisheni kwenda kwingine.

Kusaidi kazi za Umisheni

Wabaptist hutoa msaada wa kimisheni kwa njia mbalimbali. Makanisa hutuma sehemu ya fungu la kumi au matoleo mengine kwa mashirika ya kimisheni, kufadhili kazi yao ya umisheni na kuwasihi Wakristo kujitoa na kufanya kazi za umisheni kama Mungu amewapa huo wito wa kutumika.

Ngazi mbalimbali za dhehebu la Baptist hufadhili umisheni. Bodi ya wamisheni na umoja wao hutoa mafunzo na msaada kwa ajili ya walioajiriwa kama wamishonari na wale waliojitolea. Ngazi za kitaifa za Kanisa na makundi mbalimbali ya umoja/ushirika husisitiza kutoa msaada wa pesa na maombi kwa ajili ya umisheni. Taasis za idara ya Wanawake ziko vizuri sana kwenye kutoa elimu juu ya umisheni, maombi, kutafuta ufadhili, na kujishughjulisha na masuala ya umisheni. Vyuo vya kati, vyuo vikuu na seminari hutoa mafunzo juu ya umisheni, kufadhili warsha juu ya umisheni na kutoa kazi mbalimbali za umisheni.

Wabaptist kwa kila mmoja nao hutoa msaada kwa ajili ya shughuli za umisheni. Huwaombea na kuwatia moyo walioko kwenye umisheni, hutoa mali zao kwa ajili ya kuwasaidi wamisheni na kazi zao, na wengine hutoa hata watoto wao kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za umisheni.

Msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia kazi ya umisheni kwa Wabaptist kwa wakti wote ni wa uhiari. Japo kuwa, wito mkubwa umetolewa kwa watu ili kutoa kikamilifu kwa ajili ya kazi ya umisheni. Dhehebu la Baptist limekuja na mbinu mbalimbali za kusaidia hii kazi, kama vile kuanzisha mpango wa ushirkiano, ili kupitisha misaada ya hiari kwa wamisheni.

Changamoto za Umisheni

Changamoto zipo kwa ajili ya umisheni sasa na hata wakati uliopita. Changamoto zingine zinatoka ndani ya Baptist yenyewe. Maoni juu ya utabiri ujao  na dhana ya kujitegemea kwa Kanisa la mahali hudhoofisha kazi ya umisheni. Watu na Makanisa ambayo wana mawazo hafifu na sio kuwa na mawazo mapana juu ya ulimwengu hawawezi kuliona hili suala la Kiblia juu ya umisheni kuwa la muhimu. Ugombi ndani ya dhehebu unasababishwa Kanisa kuona umuhimu wa kazi ya umisheni na kushidwa kutoa msaada wa kusaidia umisheni.

Kwa maana nyingine, utata juu ya mwenendo wake pia huleta changamoto nyingi kutoka nje. Ukabila pamoja na ushamiri wa dini za asili huzuia wamisheni kufanya kazi zao kwenye maeneo mbalimbali. Mitazamo na imani mbalimbali potofu hudhoofisha kazi ya umisheni. Kufanya kazi ya umisheni kwenye njia ambazo sio sahihi hakuwezi kuleta ufanisi.

Labda changamoto kubwa ni uwezo wa kupata fedha za kutosha  na kukidhi mahitaji binafsi ya wamisheni wengi ambao wamesambaa ulimwenguni kote. Yesu alisema, “Mavuno ni mengi, watenda kazi ni wachache.” Huo bado ni ukweli hata sasa. Hivyo hatuna budi kuomba, kama Jesu alivyosema, kwamba Bwana wa mavuno, atatuma watenda kazi shambani mwake’. (Mathayo 9:37-38).

Hitimisho

Wabaptist wameandika na wanaendelea kuandika masomo mengi juu ya habari za umisheni. Hata hivyo, bado yapo mengi yanapopaswa kufanywa. Wabaptist wanapo fanya hii huduma, toa na omba kwa ajili ya kazi ya umisheni ulimwenguni, Mungu anao uwezo wa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya maelfu ya watu duniani kote.

“Jambo kubwa la uzushi ambalo Kanisa linaweza kuwa nalo ni kudharau na kukataa wajibu wa umisheni.”
H. E. Dana