Uhiari wa Ushirikiano kwa Wabaptisti: Changamoto na Faida

“Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu…”
I Wakorintho 3:9

Mnyororo wa mchanga wenye nguvu ya chuma….. hivi ndivyo James Sullivan, Kiongozi mashuhuri wa muda mrefu wa Baptist, alivyowaelezea suala la uhiari wa ushirikiano ndani ya Baptist. Faida ya uhiarin wa ushirikiano umeendelea kuleta faida miongoni mwa Wabaptisti waliojitoa kuuendeleza na kuuimarishwa zaidi mbele ya vikazo na changamoto.

Vikwazo kwenye Uhiari wa ushirikiano

Kwa nini iliwachukua miaka mingi Wabaptisti kufikia kwenye hali ya kuimarisha uhiari wa ushirikiano ndani ya Makanisa na hata ndani mifumo ya Baptist? Jibu lake limejikiti kwenye maeneo mawili, yaani kutokana na mafundisho ya Kibaptisti lakini pia kutokana na historia ya Wabaptisti.

Wabaptisti husadiki kwamba Biblia ndiyo yenye mamlaka juu ya mafundisho yote na destruri za Makanisa. Wabaptisti wengine wamesisitiza kwamba Biblia haijatoa mwongozo wa namna ya kusimamia mifumo kundi la waumini zaidi ya ushirika wa mahali. Hii imani inazuia Wabaptisti kuinua na kusaidia taasis za Kibaptisti zaidi ya Kanisa la mahali.

Wabaptisti wengine wanasisitiza kwamba Biblia imeeleza wazi kwa yote mawili hatua na mifano ya uhiari wa ushirikiano miongoni mwa Makanisa (Matendo 15; 2 Wakorintho 8-9; Wagalatia 1:2; 2:1-10; Ufunuo 1-3). Hawa Wabaptisti wana nia ya kuanzisha majimbo, kanda na ngazi za kitaifa kwa ajili ya umisheni, elimu pamoja na huduma za jamii.

Kizuizi kingine kinachopelekea uhiari wa ushirikiano kutoonyesha ufanisi miongoni mwa Wabaptisti ni hali ya kujikita zaidi kwenye uhuru wa Kanisa la mahali. Wabaptisti wengi walikuwa na hofu kwamba taasis zilizoanzishwa na Baptist nje ya Makanisa zitakuwa zinajaribu kuwa na mamlaka juu ya Makanisa. Hiyo basi, walisisitiza kujitegemea zaidi kuliko ushirikiano.

Kikwazo cha kujitegemea kiliwekwa wazi baada ya mkazo kwamba uhusiano wowote baina ya Kanisa na taasis unapaswa kuwa wa hiari kwa asilimia zote. Kwa uthibitisho huo, Wabaptisti binfasi wengi na Makanisa yanatamani kuanzisha hizo taasis ili kwa sababu mbalimbali.

Kikwazo kingine kilikuwa uwiano ndani ya Baptist pamoja na ushindani baina ya Makanisa. Hizi sababu bado zimefanya Makanisa mengine kutotaka kushirikiana. Hata hivyo, Makanisa mengi yako tayari kushirikiana kwa hiari, kikubwa yale masuala ya msingi yanaendelea kuwepo bila kukandamizwa, kwa ajili ya ufanisi kwenye uinjilisti, umisheni, elimu na huduma za jamii.

Faida dhidi ya Uhiari wa Ushirikiano

Baada ya kuziondoa hivyo vikwazo juu ya ushirikiano wa hiari, Wabaptisti walianzisha muunganiko mbalimbali, kama vile majimbo na ngazi za kitaifa, ili kutoa njia kwa Makanisa kuweza kushirikiana. Tangia awali, hii miunganiko haikuanzishwa kwa kutaka Makanisa yahudumie huko. Ilianzishwa ili kulihudumia Makanisa.

Taasis za dhehebu mwanzoni zilianzishwa ili kuyatumikia Makanisa kwa kuonyesha njia ya jinsi gani Makanisa yanaweza yakafanya kazi kwa pamoja ili kuonyesha dhahiri sababu ya Kristo kuja. Ushirikiano wa uhiari husaidia Makanisa kufanya zaidi ya pale Kanisa moja lingeweza kufanya ili kumdhihirisha Kristo.

Baadae, majimbo na ngazi za kitaifa walibuni namna ya kusaidia Makaninsa ili kufanya huduma zao mbalimbali kama Kanisa la mahali. Zaidi ya hapo, ushirikiano wa hiari unaweza kusaidia yale Makanisa yanayokumbwa na changamoto, kama vile ugomvi wa ndani kwa ndani na uhaba wa fedha. Kanisa linalopitia kwenye hali kama hizi linaweza kuomba msaada kutoka kwa jimbo au ngazi ya kitaifa bila kupoteza uhalisia wake wa kuwa Kanisa linalojitegemea.

Watu mbalimbali, kama vile Wachungaji na washirika nao hupata faida kwenye ushirikiano wa hiari. Dhehebu hutoa bima na aina nyingine ya misaada kwa wakati mwingine kwa wale ambao wametolewa kwenye nafasi zao bila ya kuwa na kazi nyingine ya kufanya; hii suala kila wakati linakuwa la hiari na sio suala ambalo dhehebu linahitaji lifanye.

Taasis za Baptist pia hufaidi kwenye ushirikiano wa hiari. Uhusiano wa hiari na jimbo au ngazi ya kitaifa kunaweza kupelekea hali ya msaada zaidi kwako ili kuimarisha taasis na kuipa nguvu zaidi kuliko ingekuwa taasis yenyewe inayojitegemea.

Dhehebu la Kipatisti kufaidika kutokana na uimara na nguvu zinazoonyekana kwenye mashirika mbalimbali ya Kanisa na taais zake. Huu uwanja wa kujihusisha unasaidia Waabaptisti kufanya huduma kwa ufanisi zaidi kuliko ingekuwa vinginevyo. Hivyo, kundi kubwa la watu wote ndani na nje ya dhehebu la Baptist hufaidika kutokana na ushirikiano wa hiari.

Changamoto dhidi ya  Uhiari wa ushirikiano

Japo faida za uhiari wa ushirikiano ni nyingi miongoni mwa Wabaptisti, vikwazo na changamoto vinaendelea kuwepo. Hapa ni baadhi ya hizo ambazo mara nyingi zimeweza kubainika na wale wanaofuatilia maisha ya Wabaptisti:

 • Imani iliyojengeka mwa wengine kwamba madhehebu ni mambo ya zamani. Watu hawa huona kwamba imani na mafundisho ya Kibaptisti yamepita na wakati na hayana maana na kuona upekee wa Wabaptisti kuwa hauna maana. Hivyo, huona sababu ndogo sana kushirikiana na majimbo, japo wengine hushiriki kupitia makundi maalum, mfano yale ambayo yanaundwa wakati wa kuabudu au kulingana na tofauti za kiutamaduni.
 • Uanzishwaji wingi kwa wa mashirika ya kusaidia Makanisa.Haya mashirika kwa asilimia kubwa yanafanya vizuri sana, yanatokana na watu mbalimbali kutoka kwenye madhehebu tofauti tofauti. Husaidia Makanisa kwenye maeneo yote mawili ya kulisaidia Kanisa kwenye masuala ya uendeshaji wa huduma na matakwa mbalimbali ya huduma tofauti na maswala ya dhehebu.
 • Uwepo wa Makanisa makubwa saana. Haya Makanisa yana uwezo wa kufanya mambo yao wenyewe na hata yale masuala ambayo majimbo na ngazi za kitaifa zingefanya. Kwa nyongeza, hayana shida na misaada wa aina yeyote kutoka kwenya jimbo au ngazi ya kitaifa. Hivyo Makanisa mengi ya aina hii hayajihusishi kwenye uhiari wa ushirikiano ndani ya Baptist.
 • Mwendelezo wa migogoro mbalimbali ndani ya Baptist. Makanisa mengine yanaona ni bora yasijiingize kwenye migogoro baina ya majimbo na ngazi zake na hata makundi mengine ya madhehebu, hivyo kuamua kujitoa kwenye ushirikiano wa kidhehebu.
 • Nguzu ya ziada inayotumika juu ya Makanisa kutoka kwenye viongozi wengine wa dhehebu kufuata ili kutambulika kwenye ushirikiano. Haijalishi nguvu inatumika kwa kutumia maadiko fulani, kufuata mfumo fulani wa kupata msaada wa fedha labda kwa kukubali fundisho fulani, uhalisia wa uhiari wa ushirkiano hukandamizwa.
  • Hali ya kujitegemea kifedha kwa taasis mbalimbali za dhehebu.
  Kama taasis ambazo awali zilitegemea sana msaada kutoka kwenye ushirikiano zinafikia hatua ya kujitegemea bila huo msaada. Zinaweza kujitoa kwenye dhehebu.
  • Dhana ya kusema majimbo au ngazi za juu ndio wenye mamlaka ya kulisaidia Kanisa ili kuweza kutimiza majukumu ya huduma yake.
  Kusema “mmetufanyia nini sasa?” haya mawazo yanaweza kupelekea kushiriki kwa kidogo sana kwenye ushirikiano wa hiari wa Kibaptisti wakati matarajio ya Kanisa hayajafikiwa

Majibu dhidi ya Changamoto dhidi ya Uhiari wa Ushirikiano

Changamoto zinazoonekana kwenye uhiari wa ushirikiano zinatatuliwa. Kuliko kuziacha tu, njia sahihi ni kuzikabili na kuzipatia ufumbuzi na kuelezea faida zake.

Majibu yakejenga juu ya  mawazo kwamba baadhi ya Makanisa yanahitaji ushirikiano wa kidhehebu. Zifuatazo ni baadhi ya njia zinazosaidia:

 • Kwa kushiriki kwenye jitihada za ushirikiano wa uhiari kwa Wabaptist, Makanisa huwa na nguvu zaida za kufanya na kuwa na wafuasi walikomaa ili kumshuhudia Kristo kupitia jina lake.
 • Kubaki kwenye ushirikiano, Makanisa makubwa yanatoa namna ya kusaidia Makanisa madogo ili nayo yaone faida ya huo ushirika.
 • Kwa kushiriki kwenye uhiari wa ushirikiano wa Kibaptisti, Makanisa husaidia majibu yaliyo sahihi kwenye migogoro.
 • Kuwa sehemu ya ushirikiano wa hiari ndani ya Baptist, Makanisa hudhihirisha sio tu kile ambacho Kanisa linapokea bali pia mchango wa Kanisa kwenye uinjilisti, umisheni na huduma za kijamii.

Kwa nguvu na furaha zote tusifie faida za ushirikiano wa hiari. Huduma za Baptist misheni, elimu na huduma za jamii zinasaidia watu wengi sana kupitia jina la Kristo kila mwaka. Makanisa yanajihusisha na umesheni na huduma zingine zaidi ya pale ambapo Kanisa moja lingeweza.

Hitimishi

Usirikiano wa hiari kwa kweli ni mnyororo wa mchanga wenye nguvu ya chuma, mnyororo ambao kwa maajabu umeonyesha mafanikio makubwa. Kupitia uhiari wa ushirikiano, Makanisa ya Kibaptisti yameweza kuendelea kuwa na hali ya kujitegemea huku likiendele kutoa huduma mbalimbali kwa ulimwengu kupitia Jina la Kristo.

“Kumbuka,  kwenye sehemu zetu kuu za masomo yetu juu ya imani yetu na desturi,
hatuna tofauti kama Wabaptisti. Kama Makanisa yetu madogo
endapo yatapata mtikisiko juu ya mambo yasiyokuwa na maana,
yatabakia yenyewe tu, hivyo kufanyika yaanguke na kupotea kabisa.”
Barua ya wazi kwa Wabaptisti mnamo mwaka 1840 kwa Wabaptisti wa Texas
Mwandishi  R.E.B. Baylor
kama alivyoombwa kufanya hivyo na Muungano wa majimbo ya Kibaptisti.