Mwanzo
KARIBU!
Karibu! Wabaptist wanaozungumza lugha ya Kishwahili wamebarikiwa na Mungu ulimwenguni kote kwa idadi kubwa ya waumini na kuongezeka kwa Makanisa. Kwa sababu hiyo kuna haja ya kuongeza mahitaji mengine kwa waumini wapya na Makanisa, lakini pia kwa wale waliojiunga zamani, ili kusaidia kuwa na uelewa wa kutosha juu ya Imani ya Wabaptist, mwenendo wao, na huduma pia. Huo uelewa utasaidia kuimarika zaidi kwa mchango wa Wabaptist ili kukamilisha Agizo Kuu (Mathayo 28:18-20) na Amri Kuu (Mathayo 22:37-40) ya Bwana Wetu Yesu Kristo.
Hii tovuti imekuwa ikiombewa na imeandaliwa kwa nia na lengo hilo. Inazungumzia na kutoa majibu kwa maswali kama: Wabaptist ni Nani? Wanaamini nini? Kwa nini huamini kile wanachokiamini? Wanafanyeje ili kutimiza Utume wa Kristo? Utawala wao ukoje? Kwa nini huitwa Wabaptist?
Masomo yaliyomo kwenye hii tovuti sio “tamko rasmi” la Imani na destruri za Wabaptist. Ni kweli, hakuna” tamko rasmi” la namna hiyo ambalo limewahi kuwepo. Lakini, huonyesha ni jinsi gani Wabaptist huamini kwamba Biblia ni mafundisho thabiti kwa ajili ya Imani na mwenendo wa Wakristo. Kwa kuwa msingi na uhuru ndio mambo muhimu sana kwenye maisha ya Baptist, maelezo tofauti tofauti bado yanaendelea kuwepo miongoni mwa Wabaptist. Hii tovuti imelenga haswa kuonyesha kile ambacho Wabaptist kwa pamoja wameweka wazi kama imani na mienendo yao.
Ni maombi yetu kwamba hii tovuti itasaidia na kuchochea Wabaptist kuonyesha jitihada zaidi za kumtangaza Kristo hata kwa kueneza Injili kwa watu ambao sio Wakristo ulimwenguni kote.