Wabaptisti na Ushirikiano wa Hiari

“……Kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao,
wakituomba sana pamoja na kutusihi
kwa habari ya neema hii, na shirika hili
La kuwahudumia Watakatifu.”
2 Wakorintho 8:3-4

Wabaptisti wanaamini kwamba Biblia inafundisha kuwa Makanisa yanapaswa kuwa huru, kwa maana ya kusema, kutotegemea jambo lolote kutoka nje iwe ni watu binafsi au kikundi fulani. Wabaptisti pia huamini dhamana ya kwamba Wakristo wanapaswa kujihusisha kwenye umisheni, kwa kutii wito wa Kristo wa kuipeleka Injili kwa watu wote. Ushirika mmoja, haijalisha ukubwa wake, hauwezi ukatimiza vema huu wajibu kwa ufanisi zaidi.

Hivyo basi, Wabaptisti wa kwanza walikuwa njia panda bila kujua la kufanya: kwamba itakuweje kwa Shirika ambazo zinajitegemea kutimiza huu wito wa Yesu Kristo wa kuipeleka injili kwa ulimwengu wote bila kuyahusisha Makanisa mengine ambayo wangedharau dhana ya kuwa Kanisa huru?

Baada ya miaka kadha ya maombi ya nguvu, Wabaptisti wakaja na jawabu juu ya hili swali kwamba “ushirika wa hiari” miongoni mwa Wabaptisti wenyewe na Makanisa ya Baptist ndio jawabu.

Kiongozi mmoja wa Jimbo la Baptist James L. Sullivan alifananisha na “mnyororo wa mchanga wenye  nguvu ya chumal.”

Msingi wa Ushirikiano wa HIARI

Ushirika wa hiari pia ni moja ya nguzo imara kati ya msingi wa mafundisho ya Baptist. Uhiari na uhuru vimetoa upenyo kwenye uhalisia wa Baptist juu ya mafundisho na mwenendo wao. Kwa mfano, Wabaptisti huamini yafuatayo:

Biblia inafundisha suala la kupata wokovu katika Kristo ni la hiari. Imani hailazimishwi. Wokovu huja kwa njia ya imani kupitia zawadi ya neema ya Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo. (Waefeso 2:8-10). Hakuna mtu anaeweza kuchukua huu uamuzi kwa niaba ya mwingine. Hakuna awaye yeyote anayeweza kumwamrisha mwingine achukue hiyo hatua.

Ubatizo ni uthibitisha kwamba mtu mwenyewe kwa hiari amefanya maamuzi ya kumpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi. Agano Jipya linaeleza kwamba ubatizo usilazimishwe bali wakati wowote kiwe kitendo cha uhiari kama ishara ya kusema mhusika ameamua kumfuata Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi.

Uamuzi wa mtu kujiunga na Kanisa pia unapaswa kuwa wa hiari. Kulingana na Agano Jipya, ni wale tu kwa hiari waliomwamini Yesu ndio wanapaswa kuwa waumini wa Kanisa. A. Zaidi ya hapo, asiwepo yeyote wa kulazimishwa kuwa mshirika wa Kanisa.

Msaada wa fedha kwa Kanisa unapaswa kuwa wa hiari. Uhiari wa kutoa fungu la kumi na matoleo mengine, fedha kwa ajili ya kodi, zisitumike kufadhili Kanisa.

Hali ya uhiari kwa Makanisa pia huonyesha uhusiano wa Makanisa yenyewe kwa yenyewe na kwa kwa maeneo mengine ambayo ni sehemu ya dhehebu la Kibaptisti.  Kila Kanisa lina uhuru na kwa maana hiyo liko huru chini ya ukuu wa Kristo na kuamua masuala hayo kama ni nani anapaswa kuwa kiongozi wake, ni ibada ya aina gani itafanyika na jinsi itahusiana na Wabaptisti wengine. Hakuna awaye yote, shirika la dini, au mamlaka ya serikali kuwa na mamlaka ya kudhoofisha huu uhuru.

Misingi ya Uhiari wa USHIRIKA

Biblia imeweka wazi juu ya suala la uhiari wa ushirikiano baina ya Makanisa. Agano Jipya ina mifano mbalimbali juu ya ushirikiano huo miongoni mwa Wakristo wa kwanza na Makanisa. Ushirikiano ulilenga kuleta utendaji na ufanisi bora wa huduma kwa jamii, kwa ushirika na kwa kuleta ufanisi zaidi kwenye umisheni na uinjilisti.

Kwa mfano, Mtume Paulo aliwaandikia Waraka Kanisa la Wakorintho juu ya mahitaji ya Wakristo Yerusalem na kutoa wito kwa Wakorintho kuungana na Makanisa mengine ili kwa hiari kufanya makusanyo na kusaidia mahitaji ya Wakristo walikuwa wakihitaji msaada. Aliweka wazi kuwa hayo matoleo ni ya hiari. Hakutoa amri ya kufanya hivyo. Hakuna ulazima uliokuwepo. (2 Wakorintho 8:9).

Agano Jipya pia imeandika maswala mbalimbali ambayo yaliachilia mgawanyo wa jitihada za Wakristo wa kwanza juu ya masuala waliokuwa wakishughulikia na walitumia ushirikiano wa hiari ili kufanya mazungumzo yao.   Halikuwepo Kanisa hata moja au kundi moja ambalo lilitaka kuamrisha wengine wafanye kile walichokuwa wakitaka kuamini, lakini waliweza kuibua makubaliano baada ya maombi ya nguvu. Haya hayakuwa maamuzi ya kuamriwa bali yalikuwa maamuzi ya mazungumzo kwa njia ya neema. (Matendo 15). Mfano mwingine wa uhiari wa ushirikiano kwenye Agano Jipya ni makubaliano juu ya baadhi ya Wainjilisti na Wamisheni kupewa jukumu la kuwahudumia watu walio kwenye  makundi tofauti tofauti. Wengine walishughulika na jamii ya Kiyahudi na wengine walishughulikia na jamii ya watu wa Mataifa (Wagalatia 2:1-10).

Agano Jipya pia huonyesha Makanisa ya kwanza yaliyokuwa kwenye eneo moja la kijogirafia yalikuwa na mahusiano mazuri baina yao. Mtume paulo aliandika, ‘Kwa Makanisa yaliyoko Galatia” (Wagalatia 1:2). Ufunuo aliyopewa Yohana ulielekezwa kwenye Makanisa saba yaliyokuwa Asia ndogo, kila Kanisa lilijitegemea lakini yaliweza kushirikiana na mengine. (Ufunuo 1-3).

Asili ya Uhiari wa Ushirikiano

Asili ya uhiari kwenye maisha ya Baptist, chimbuko lake ni mafundisho ya Biblia, ni hakika ni ya nguvu. Hata hivyo, hali ya kujitenga na kujitegemea kabisa kwa Kanisa la mahali kuna maana ya kwamba Kanisa linakosa nguvu ya uwepo wa Kristo ndani yake ambayo hufanywa na kundi la Makanisa. Lakini ni kwa namna gani umoja unaweza ukawa na faida bila kutoa gharama ya uhiari na uhuru?

Wabaptisti wamejibu hilo swali kwa njia ya uhiari wa ushirikiano baina ya Makanisa, kupitia njia ya kawaida za kuunganisha Makanisa kwa pamoja, na kupitia makundi au mifumo mbalimbali kama majimbo kanda na taifa. Hata hivyo jawabu lake lilianza kuonekana taratibu taratibu, kwa maana kubwa ya kusema kwa sababu ya Baptist kuzuia mashirika ya kidini kuwa juu ya Ushirika wa Kanisa la mahali la waumini.

Hatua ya kwanza ambayo Wabaptisti waliifanya ili kuwa na uhiari wa ushirikiano  ni uanzishwaji wa majimbo kwenye Makanisa. Jimbo la Philadelphia lilianzishwa mwaka 1707.  Baadhi ya watu kutoka Makanisa ya Baptist walikutana na kuanzisha huu umoja usio rasmi kwa kufuata aina ya umoja ambao ulianzishwa awali huko Uingereza. Wale walioanzisha majimbo waliweka bayana kwamba hayana mamlaka juu ya Makanisa. Majimbo yalikuwepo kwa lengo moja tu la ushirika na kujadili masuala mbalimbali yanayolikabili Makanisa. Leo hii, mamia kwa hayo majimbo yanaendelea kufanya kazi, japo yanatofautiana kwenye utendaji, lakini kila jimbo hufuata mfumo wa uhiari wa ushirikiano bila kuwa na mamlaka juu ya Kanisa.

Hatua ya pili juu ya uhiari wa ushirikiano ni kuanzishwa kwa mifumo ya Kikanda. Hizi Kanda zilikuwa na mtazamo mmoja tu, kama vile kutuma wamisheni nje ya nchi, kutuma wamisheni ndani ya nchi au kuanzisha taasis za machapisho. Watu binafsi au kundi la watu walijiunga kama wanachama kwa kuchangia  fedha kwenye Kanda. Uanachama ulikuwa na wa hiari tu. Wabaptisti wanayo haki ya kusaidia au kutosaidia. Kanda bado zinaendelea kwenye maisha ya Kanisa la Wabaptisti, lakini kwa mfumo mwingine ni uanzishwaji wa ushirikiano ngazi ya kitaifa.

Muundo wa mfumo  ngazi za kitaifa ulianzishwa Marekani mnamo miaka ya mwanzoni mwa 1800. Ngazi ya taifa ni tofauti na ngazi ya Kanda kwa maana kwamba ngazi ya Kitaifa hutafuta msaada na kukusanya kusaidia jitihada mbalimbali za dhehebu, kama vile umisheni, elimu, kutoa msaada na machapisho ni zaidi ya kujishughulisha na suala moja. Idadi kubwa ya majimbo na ngazi ya Kitaifa vilianzishwa. Mpango wa ushirikiano ulianzishwa kama njia ya kusaidia kufadhili huduma za Kibaptisti, kama vile shule, vituo vya kulelea watoto na watu wazima, taasis za afya, na taasis za majimbo, kanda, kitaifa na huduma za umisheni kimataifa.

Hizi ngazi za juu kitaifa hazina mamlaka kwenye Makanisa. Taasis zingine huwa na jina kama la huu umoja wa kitaifa kama vile “ushirika” au “muungano”

Hitimisho

Ushirikiano wa uhiari miongoni mwa masuala mbalimbali ndani ya dhehebu la Baptist hutoa njia ya utendaji uliotukuka kwa kutimiza kusudi la Kristo. Makanisa kwa uhiari wake hushirikiana yenyewe kwa yenyewe kupitia miundo ya umoja kama vile majimbo au kanda, ili kuweza kutimiza huduma mbalimbali kwa upana zaidi kuliko vile Kanisa moja lingeweza kufanya lenyewe. Sehemu ya masomo itakayofuata kwenye haya mafundisho tutajadili uzuri wa uhiari wa ushirikiano na changamoto zake.

“Moja ya hatua ya msingi ni kufanya kwa hiari……
dhehebu limeunganika kwa pamoja na mifumo ambayo sio imara,
lakini uzoefu wa kutosha, mafundisho, na makusudio,
hufanya muungano kuwa imara kama chuma.”
James L. Sullivan
Mnyororo wa Mchanga wenye nguvu ya Chuma