Wabaptist na Uinjilisti

“Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”
Warumi 10:17

Wabaptisti wamejitoa kwa ajili ya Uinjilisti, kushuhudia habari njema za Yesu Kristo ili na wengine waweze kumpokea na kumwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi. Kujitoa kwa ajili ya uinjilisti ni jambo la kipaumbele kwenye kila maisha ya Baptist.

Msingi wa Uinjilisti

Uinjilisti sio kwamba ni jukumu tu la kawaida bali ni eneo lenye maana sana la kuonyesha kuwa Wabaptisti ni watu gani. Mkazo wa Baptist juu ya uinjilisti hautokani na jambo jingine bali zaidi ya mafundisho na mwenendo wa Baptist jambo ambalo linaendelea kuonyesha utofauti wa Wabaptisti na wengine.

Kwa mfano, imani juu ya ukuu wa Kristo ni nguzo imara kwenye mafundisho ya Baptist. Kwa sababu Yesu ni Bwana, wale wanaomfuata wanapaswa kufanya kama anavyo waamuru kufanya. Yesu aliagiza, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19). Aliendelea tena kwa kusema, “nanyi mtakuwa mashahidi wangu” (Matendo 1:8). Amri Kuu ya Yesu (Mathayo 22:36-40) inatoa wito wa kuhubiri habari njema ya Kristo, upendo kwa majirani ni pamoja na kuwashirikisha habari za wokovu katika Kristo.

Kwa Wabaptisti, Biblia ndiyo yenye chanzo cha mamlaka juu ya mafundisho ya dini na maisha ya Mkristo. Biblia inafundisha juu ya wokovu kwamba ulipatikana kutoka kwenye nguvu ya kuishinda dhambi. Kutoka jehanamu kwenda mbinguni, huja kupitia imani kama zawadi ya neema kutoka kwa Mungu kwa kumtoa Mwanae, Bwana Yesu Kristo (Yohana 3:16-18; Waefeso 2:8-10).  Biblia imenukuu usemi wa Yesu, “ Mimi ni njia, ukweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” (Yohana 14:6).

Wokovu haupatikani kwa kufanya matendo mema, au kwa njia ya sakramenti, au kwa ubatizo, au kwa kuwa mshirika wa Kanisa lakini ni kwa itikio la imani kwa neema yake Mungu ya wokovu kupitia Yesu Kristo. Hivyo, Biblia pia husisitiza umuhimu wa kutangaza habari njema ili watu wamjue na kumwamini Yesu na kuokolewa (Warumi 10:13-17).

Wokovu ni kuwa na uhusiano na Yesu Kristo. Wabaptist huamini kwamba Biblia inafundisha kuwa wokovu ni suala la kitendo, kinachotokana kwa mtu kutubu dhambi na kumwamini Kristo kwa imani. Yesu alifananisha hiki kitendo kama kuzaliwa kwa mara ya pili (Yohana 3:7). Hiki kitendo sio cha kusukumwa bali ni mamuzi binafsi, hakuna awezaye kufanya hili kwa niaba ya mwingine.

Biblia inafundisha kwamba injili ni kwa wote, kwamba atakayemwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wake basi atapata wokovu (Yohana 3:16; Warumi 10:13). Hivyo basi, watu wote wanaombwa kumwamini Kristo kama Mwokozi na kumfuata yeye kama Bwana.

Njia za Kufanya Uinjilisti

Kwa sababu ya umuhimu wa uinjilisti, Wabaptist wanafanya kila linalowezekana kuwafikia watu na habari za kumwamini Yesu. Kulazimishwa kwa namna yeyote ile sio njia sahihi ya kumfanya mtu amfuate Yesu.Yesu hakulazimisha watu wamfuate (Mathayo 19:16-22). Ili kuwa halisia, mwito wa kuikubali injili unapaswa kuwa wa hiari na huru. Hivyo basi, Wabaptist husisitiza kwamba pande zote mbili, yaani anayepeleka injili na anayepokea wafanye kwa hiari.

Wabaptist huamini kwamba suala la uinjilisti ni nafasi na wajibu wa kila muumini kulifanya. Japo wengine wamepewa kalama ya uinjilisti na Mungu (Waefeso 4:11), wafuasi wote wa Yesu wanapaswa kueneza injili. Japo moja wapo ambalo Biblia inaelezea kama jukumu la kuhani muumini ni kwamba kila kuhani aliyeamini anapaswa kutoa huduma ya kuieneza injili katika upendo kwa watu wengine, sio tu Wachungaji, Wamisheni na Wainjilisti.

Mtu anapochukua nafasi ya kuieneza injili kwa wengine ni jambo njema kwa uinjilisti. Wabaptist wanao wajibu kwa kujikita katika maombi na kuwashuhudia watu wengine juu ya maisha yao binfasi kuhusu imani yao kwa Kristo, kwa maneno mengine, kuwa shudhuda (Matendo 1:6-8). Makanisa, majimbo, kanda na ngazi ya kitaifa ya dhehebu hutoa warsha na mafunzo maalum ya namna ya kutia moyo na jinsi ya kuwa mashuhuda (kufanya uinjilisti).

Sehemu nyingine ya shuhuda wa mtu binafsi ni kuishi maisha ya Kikristo, jambo ambalo huwavutia wengine kuipokea injili. Hata hivyo, wabaptist hutambua kwamba sio tu namna aina ya maisha kuwa ndio njia yakujitosheleza kwa watu kuipokea injili: maisha ya bila dhambi ya Yesu, sadaka aliyotoa kwa njia ya kifo, kufufuka kwake na umuhimu wa kumwamini na kumpokea Yeye ni kupata wokovu. Maneno ni muhimu (Warumi 10:8-17). Uinjilisti ni pamoja na kuieneza injili kwa maneno na kwa matendo pia.

Kuhubiri injili (2 Timotheo 4:2) ni njia nyingine ambayo Wabaptist hutumia kufanya uinjilisti. Kuhubiri kwenye ibada mara nyingi mkazo unakuwa kwenye uinjilisti hata kama mahubiri yanahusu masuala mengine. Wabaptist huhubiri kwenye ibada maalum za uinjilisti, nje ya majengo ya Kanisa kwenye uwanja wa wazi na hata kwenye makumbi mbalimbali kwa kuwasihi watu kumwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao.

Mafundisho  (Mathayo 28:20)  Teaching (Matthew 28:20) na Wabaptist pia hubeba ujumbe wa uinjilisti. Kwa mfano, Wabaptist huamini uwepo wa shule ya Jumapili hulenga mambo mawili – kujifunza Biblia na uinjilisti. Vipindi vya kujifunza kwenye shule za Biblia, warsha na makongamano hubeba ujumbe wa uinjilisti ndani yake. Shule za Kibaptist zipo sio kwa ajili ya kutoa elimu bali pia kwa ajili ya uinjilisti.

Huduma kwa jamii (Mathayo 25:31-46) kwa Wabaptist pia hulenga mambo mawili – kuwapatia mahitaji yao ya kila siku, kimwili na kuwaenezea injili. Wabaptist huamini kwamba mahitaji pekee hayatoshi mpaka uhitaji wa kimwili na kiroho utakapokamilika.

Wabaptist wanazo taasis maalum na vikao mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha na kukuza uinjilisti. Kwa mfano, Ngazi za majimbo, kanda na hata kitaifa zimeweza kuanzisha idara mbalimbali zenye watumishi wengi ambao kusudi lao ni kufanya na kuratibu masuala ya uinjilisti, na kuwa na makongamano ya kuwashawishi na kuwaelekeza jinsi ya kufanya uinjilisti kwenye kama Baptist. Kwa mtazamo huo huo, seminari mbalimbali za Kibaptist zina wakufunzi waliobebea ambazo walifunzu na kufundisha somo la uinjilisti.

Kuwaombea Wakristo ili kwa ujasiri kuieneza injili (Matendo 4:31) na kwa watu ili kuwa na imani kwa Bwana Yesu Kristo na kuokolewa kitendo ambacho kinaonyesha matokeo mazuri kwenye jitihada za uinjilisti, ni dhahiri maombi yanapaswa kuwa ndio nguzo kwenye suala la uinjilisti.

Vikwazo na Changamoto za Uinjilisti

Mkazo na jitihada za Wabaptist kwenye uinjilisti sio kwamba hakuna vikwazo na changamoto. Kwa sababu ya umuhimu wa kufanya uinjilisti kwa kuwasaidia watu kuupata wokovu, shetani nae atajalibu kudhoofisha hico jitihada.

Kutojali na tofauti zilizopo miongoni mwa Wakristo ni moja ya vikwazo kwenye suala la uinjilisti. Sababu zinazochangia hiyo hali ni nyingi, kama vile uchanga wa kiroho, uelewa mdogo wa Kibiblia na hali ya ku kengeuka.

Hofu nayo ni moja ya kikwazo kwenye uinjilisti. Watu wanaweza kuhofia kushindwa, kunyanyaswa, kukataliwa na hata kujibiwa kwa kejeli wakati wa kufanya uinjilisti. Hivyo vikwazo vinaweza kuondolewa kwa kutambua kwamba Roho Mtakatifu anayo nafasi kubwa kwenye uinjilisti (Matendo 4:31). Yesu aliahidi kwamba Roho Mtakatifu atawapa nguvu “nanyi mtakuwa mashahidi wangu” (Matendo 1:8). Roho Mtakatifu, sio mtu anayeshuhudia, huleta uthibitisho na kujitoa ndani ya moyo wa mtu aliyepotea.

Mashaka juu ya upekee wa Kristo kwa kuuleta wokovu kunaweza kudhoofisha uinjilisti pia. Kuna mambo matatu ambayo hufundishwa juu ya kupata wokovu. Imani ya usawa (ni imani ambayo husema kila mmoja ataokolewa), Imani ya uwiano (ni imani ambayo husema Kristo ni hatua ya kuelekea na sio njia ya kupata wokovu) na Imani ya vitu( imani hii husema hakuna kitu ambacho kimewahi kuweko isipokuwa hewa tu hivyo hakuna wokovu wa kiroho) ni mambo ambayo hudhoofisha uinjilisti.

Hitimisho

Wabaptist ni watu wa uinjilisti kwa sababu ya msingi wa imani yao na hutumia njia mbalimbali ili kueneza Habari Njema za Yesu Kristo. Ni kweli kuna makwazo na changamoto hudhoofisha hii huduma ya uinjilisti. Kwa njia ya maombi na kukua katika Kristo, ushindi unaweza kupatikana, na uinjilishi unaweza ukaenea zaidi na zaidi an kuwa na matunda mazuri.

“Kazi kubwa ya uinjilisti………inapaswa kufanywa na Kanisa kama Kanisa, na kwamba kwa kadri inayowezekana kila mshiriki wa Kanisa anapaswa kuwa sehemu ya hilo,”