Wabaptist: Kuabudu

“Njooni, tuabudu….”
Zaburi 95:6

“Wabaptist ni ‘Watu wa Kanisa huru’
Hupata furaha kwenye aina mbalimbali ya mitindo
ya jinsi ya kuabudu na kuenenda kwenye Makanisa yao….”
William R. Estep,
Kwa nini Mbaptist? Masomo ya Imani ya Baptist na Urithi

Neno “kuabudu”  limetokana na neno la zamani la Kiingereza. Kuabudu ni kudhihirisha kwa neno na matendo kwamba Mungu anatosha juu ya upendo wake kwetu, kujitoa kikamilifu na utiifu kamili kwa kila eneo la kuishi kwetu (Ufunuo 5:12).

Asili ya Kuabudu

Tunakiri kwamba Mungu anatosha kwa ajili ya kujitoa kwake na kuishi kwetu kila siku (Warumi 14:8). Tunaonyesha upendo wetu kwa ajili ya Mungu kwa yale tunayofanya kwa kuwahudumia wengine kwa njia ya uinjilisti, umisheni, huduma mbalimbali na jitihada za kuufanya ulimwengu wote kuwa na ubinadamu.

Wabaptist huendeleza hizi hatua mbalimbali za kuabudu. Wabaptist pia huamini kwamba kuna nyakati za kuabudu ambapo mtazamo wetu wote ni juu ya Mungu na uhusiano wetu na Mungu. Hizo nyakati hutoa nafasi ya kuonyesha kujitoa na kumpa sifa Mungu, kwa kutubu dhambi na kuomba msamaha kutoka kwa Mungu, kutoa shukrani kwa Mungu na kupeleka mahitaji yetu mbele zake Mungu.

Hivyo Wabaptisti wamethamini umuhimu wa ibada binafsi, kwa familia kuabudu majumbani, na kuabudu kwa ushirika kwenye Makanisa. Kila hatua zinapaswa kufanywa kwa uhuru.

Kuabudu kwa Ushirika

Wabaptisti huamini kwamba kuabudu kwa ushiriki ni kiungo muhimu kwenye maisha ya Kanisa (Waebrania 10:25). Agano Jipya halitoi utaratibu maalum kwa ajili ya kuabudu kwa ushirika lakini huonyesha mifano jinsi gani Wakristo wa kwanza waliweza kuabudu.

Dhehebu la Baptist halitoi mwongozo fulani wa kufuata wakati wa kuabudu kwenye Makanisa – au aina nyingine yeyote, kwa ajili ya hilo. Kwa kufuata uongozi wa Biblia, kila ushirika uko huru kuamua njia ambayo kwao wanaona ni bora zaidi. Njia za kuabudu kwenye shirika za Kibaptist hutofautiana Kanisa kwa Kanisa, lakini baadhi ya taratibu kila mara zinafuatwa na zinakuwa sawa, uhuru wa kuabudu ndio uufunguo kwa hayo yote.

Siku na muda wa kuabudu kwa ushirika hutegemeana  miongoni mwa Wabaptisti. Hata hivyo, Wabaptisti walio wengi hufanya ibada zao siku ya Jumapili (Matendo 20:7’ 1 Wakorintho 16:2). Idadi ya ibada na muda wa ibada pia hutofautiana miongoni mwa Makanisa.

Viongozi wa ibada hutegemeana. Kwenye ibada maalum Mchungaji huongoza ibada na kuhubiri, kiongozi wa sifa anaongoza sifa, baadhi ya waumini wa ushirika au viongozi wa Kanisa huongoza maombi ya pamoja, hushuhudia na au wanakusanya matoleo. Viongozi wa ibada wako huru kuvaa vyovyote vile ambavyo ushirika huona ni sawa.

Biblia ndio Msingi kwenye Ibada za Kibaptist  (2 Timotheo 3:15-17).  Dhehebu la Baptist halina mamlaka ya kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia Biblia. Makanisa yapo huru kutumia aina ya chapisho la Biblia, maandiko gani ya kusoma na ni kwenye kipindi gani kwenye ibada Biblia husomwa. Kusoma Biblia kwa mmoja mmoja au wote kwa pamoja ndani ya ibada yote hufanywa. Maombi ni msingi kwa ibada zote kwa Wabaptisti, yote maombi binafsi au maombi ya pamoja (Marko 11:17; Wafilipi 4:6). Hakuna mwongozo wa maombi ya kidhehebu. Mara nyingi Mchungaji huongoza “maombi ya kichungaji” ambayo yanaweza kuandikwa lakini kwa kawaida hutamkwa tu.

Hubiri ni sehemu muhimu ndani ya ibada za Baptist (Matendo 20:7-9; 2 Timotheo 4:2). Kuhusu mahubiri, mhubiri yuko huru kuchagua kicha, lengo, aina na andiko la kusoma. Dhehebu halina mwongozo wa aina yeyote juu ya hili. Aina ya kuhubiri pia ni juu ya mhubiri mwenyewe; wengine husoma kwenye machapisho wakati wengi huhubiri kutokana na kile walichokiandaa kama kumbukumbu au kwa kufafanua kutoka kwenye andiko moja kwa moja.

 Uimbaji una umuhimu wake  Ibada za Baptist (Zaburi 100:2; Waefeso 5:19). Pia uhuru ni muhimu. Japo kwa uhalisia Makanisa yote washiriki hushiriki kwenye uimbaji, aina ya nyimbo zinazoimbwa huleta maana sana. Zaidi ya kuimba kama ushirika kwa pamoja, uimbaji kwa njia ya vikundi vya kwaya, vikundi vya kusifuv waimbaji binafsi na vikundi vya uimbaji kwa pamoja ni mambo ambayo yanaweza yakawemo kwenye ibada ya Baptist. Aina ya vyombo vinavyotumika pia ni jambo la maana sana, ikiwa ni pamoja na kinanda, ma gita na vyombo vingine vya muziki pia.

Kushuhudia ni jambo la kawaida  kwenye ibada za Baptist. Aina ya ushuhuda hutegemea na mhusika alivyoona ashuhudie na kwenye msisitizo kwa kile ambacho Kanisa linafanya kwa wakati huo.

Utoaji wa sadaka unakuwepo  kwenye ibada hizo (1 Wakorintho 16:1-2). Makanisa ya Baptist huendeshwa kwa zaka na matoleo mbalimbali yanayotolewa kwa hiari.

Wito wa kufanya maamuzi ni nafasi muhimu kwenye ibada ya Wabaptisti, kama kwa wale waliopotea ili wamwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi,  njia ya kupokea wanaojiunga na Kanisa iwe kwa “barua” au kwa “kukiri tu”, kuwapokea walirudi nyuma ili kumrudia tena Kristo na kwa watu kuonyesha “kujitoa kwa hiari” kwenye huduma mbalimbali. Kwa kawaida watu hupaswa kufanya hayo maamuzi mbele ya umati wa watu, kwa kwenda mbele ya madhabahu kutamka na kwa kawaida husindikizwa na “wimbo wa mwaliko” lifuata neno/hubiri kwa ufupi.

 Ubatizo na Meza ya Bwana vinaweza kuwepo  kwenye ibada. Pia, kila ushirika uko huru kuchagua lini na jinsi gani ya kuendesha haya maagizo makuu mawili.

Ibada inaweza ikafanyika mahala popote paleworship. Hata hivyo, ibada za juma hufanyika kwenye majengo maalum ambayo kusudi lake ndio hilo.

Aina ya majengo ya kuabudia ni muhimu  kutokana na matakwa na uchumi wa Kanisa. Utaratibu wa kukaa kwa kawaida ni kwamba watu hukaa kwa kuitazama meza inayotumika kwa ajili ya meza ya Bwana iliyoko mbele ya miambari, wakati mwingine ikiwa na Biblia juu yake, huku kisima cha ubatizo kikiwa nyuma ya miambari. Huu mpangilio huachilia ukuu wa Neno la Mungu kwenye ibada na umuhimu wa haya maagzio makuu mawili, ubatizo na meza ya Bwana.

Ibada na Mikazo Mingine ya Baptist

Ibada za Kibaptisti zinahusiana kwa ukaribu sana na mafundisho mengine ya Kibaptisti na uthamani wake. Kwa mfano, imani juu ya ukuu wa Kristo huongoza imani ya Baptist kiasi cha kwamba kwenye ibada Makanisa yanapaswa kumtazama Yesu na kutafuta na kufuata kusudi lake kwa Kanisa.

Mafundisho ya Baptist juu ya kutambua mamlaka ya Biblia juu ya imani na mwenendo hujidhihirisha kwenye ibada kwa kuisimamia Biblia. Kwa sababu Biblia ni kitabu kutoka kwa Mungu na juu ya Mungu kinapaswa kuwa na nafasi muhimu nkwenye kumwabudu Mungu. biblia ndio msingi wa maombi, mahubiri na nyimbo.

Mafundisho ya Biblia juu ya ukuhani wa waumini (1 Petro 2:5; Ufunuo 1:6; 5:10), uweza wa roho, uongozi shirikishi wa Kanisa la mahali na kujitegemea (Matendo 6:1-6; 13:1-3; 2Wakorintho 8:1-8) . Hukubaliana na mafundisho ya Baptist kwamba kila muumini anao uwezo kuongoza ibada na kila Kanisa la mahali chini ya ukuu wa Kristo linapaswa kuwa huru kuchagua mahali, aina na viongozi wahusika kwenye ibada.

Mafundisho ya Biblia kwamba wokovu hupatika kwa neema kupitia Kristo (Waefeso 2:8-10) huongoza wa Baptist kwenye kumwabudu Mungu kiasi cha kwamba hakuna jambo lingine ambalo linaweza likaweko kwenye ibada kama njia ya kupata wokovu zaidi ya hiyo imani.

Uhuru wa kuabudu (Wagalatia 5:1) ni jambo lingine ambalo linaleta mwanga kwenye suala la kuabudu ndani ya Baptist. Ili kuwa na uhalisia, kuabudu kunapaswa kuwa huru, kusishurutishwe. Makanisa yanapaswa kuwa huru ili kuchangua, muda, na aina ya ibada. Kwa sababu ya kutambua dhahiri juu ya uongozi wa Roho Mtakatifu ndani ya Baptist (Wagalatia 5:18), huo uhuru usiwe chanzo cha kuleta machafuko, bali mambo hupaswa kufanywa kwa “weledi na utaratibu” (1 Wakorintho 14:40).

Hitimisho

Ibada za kumwabudu Mungu kwa Wabaptist hutofautiana sana miongoni mwa Makanisa lakini baadhi ya taratibu ziko sawa kwa sababu ya mafundisho ya msingi ya Kibaptist. Haijalishi kwa namna gani, lakini kumwabudu Mungu ndani ya Baptist kunapaswa kulenga kumwinua Mungu na sio kitu kingine.